Monday, December 14, 2015

cheka kidogo


Enzi zetu

Enzi zetu ilikuwa raha sana, najua mtabisha maana
mnajiona wajanja, lakini aise mmekosa mengi
sana. Siku hizi shida tupu, nikikumbuka enzi zetu
nawaonea huruma.
ule kwetu enzi zile ukitaka kuoa, unapeleka posa
ikikubaliwa unapangiwa mahari, mara nyingi
mahari ilikuwa ng’ombe wawili, mbuzi na kondoo
mmoja, raha yake ilikuwa baba yako ndiye
anayekulipia mahari.
Bibi harusi alikuwa hana gharama kabisa, akijitahidi
kununua gauni lolote jeupe na kilemba cheupe,
kamaliza vazi la harusi na bwana harusi hapo
kuonesha unajali unajitahidi unamnunulia
mchumba raba nyeupe, mchezo unakwisha
hudaiwi kitu.
Siku ya harusi huna haja ya gari wala baiskeli, bibi
harusi anatembea kwa mguu toka kwao mpaka
kwako, mnaanza maisha, mambo simpo kabisa.
Ng’ombe walipoanza kuwa shida hasa kwa watu
wa mjini, ndiyo ikaanza taratibu ya kulipa fedha
badala ya wanyama kama mahari, ng’ombe
alikuwa shilingi mia tano, mbuzi na kondoo shilingi
thelathini.
Ukipangiwa mahari ya ng’ombe wawili na mbuzi
wawili unalipa shilingi alfu moja na sitini, tena kwa
kawaida mahari huwa haikamilishwi, hivyo
ikikushinda kidogo hakuna kesi.
Sasa zama hizi kiboko, mtu unapangiwa mahari
shilingi milioni mbili, halafu lazima utafute suti ya
laki tano, magari ya kifahari, mipombe,
ukumbi, mivideo, kitu kama milioni kumi lazima
zikutoke. Halafu kuna
hiki kichekesho kipya cha kuleta mizawadi kwenye
ukumbi, vitanda
makabati mafriji, mafriza.
Vurugu tupu. Wiki moja baada ya harusi
maharusi wako hoi kifedha wanaanza kukopa hata
hela ya kula. Acha
bwana enzi zetu ilikuwa raha sana.

Hataree

Inakuwa nene masela wangu? Kipande hii ni mzuksi
kichizi arifu. Kama vipi welikamu kwa sana kwa fasi
ya hapa jamvini tukisanue mazee ama nini! Basi
sawa.
Wanangu kuna ishu zingine hazihitaji mtu kuwa
machi noo kozi kuna pipo ni mamasta maindi ileile
na ukileta za kujua sana dheni watu wanakupiga
chabo dheni wanakuchora tu si unajua zile? Kuna
wale makaksi wa ukwehe ambao mara nyingi siyo
wachangiaji wa mamada kiivo bati wana madini ile
mbaya kwa kichwani! Ebana kitu cha holidei ya
uhuu vepe? Mambo ya foto kanga na ekotite
yalikuwa mpango mzima? Barida!
Basi bana huku na huku selaa wangu akamingo na
chiki mmoko mkare aibu kiaje sasa mazee. Yaani
usipimie kabisa kwa jentromani wa ukwehe achana
na wale watoto mayai lazima uzime fegi kachala
wangu.
Siyo siri wanangu mtoto ni sumu ile mbaya sema
tu laifu lake huko nyuma lilikuwa la kukurukakara
za hapa na pale wanangu wenyewe kwenye
mambo yaleee ya kubadili mameni kama chizi
f’lani hivi freshi.
Laifu limemuvu fasta na huwezi kubilivu si ndo
msimu wa kitu cha holidei? Masela hii siyo taimu
ya kumbwela ni mwendo wa maandalizi ya kufa
mtu ili wanangu wasiaibike.
Unaambiwa jamaa yangu kazama ofisini kwa shori
hapo dauni tauni Bongo tambarare kupata sevisi
f’lani si ndo kachaa kadata na mtoto? Akaona
isiwe kitu, baada ya kitambo f’lani hivi mwana
akatangaza kuweka kitu na boksi ndani.
Sasa bana unajua ukitaka kugonga bata la holidei
usimchunguze sana kozi hutalila kwa raha au
hutalila kabisa. Basi bana, kabla ya kumweka kwa
skani akaona amwekee spai wa kumchunguza
kama ametulia au ndo kama hivo magumashi?
Yule msela aliyepandikizwa na mwana si ndo
akaanza mbishe za kumfukuzia shori? Kama
nilivyokuteli bifoo kwamba tabia ni kama rangi
kuifuta ina kosti zake. Jamaa kamuimbisha shori
hadi wakakubaliana wakafanye yao kwa hoteli!
Da! Noma sana wanangu! Shori amefika kwa
mapokezi kakaribishwa freshi na bashasha za
kumwaga kisha akapewa funguo za rumu.
Mazee wakati shori anamsikilizia jamaa akiwa
amejimwaga kwenye peji ndani ya suti ya kuzaliwa,
ghafla bin vuu mlango ukagongwa…kwenda
kufungua shori hakuamini macho yake kukutana
feisi kwa feisi na mchumba’ke orijino kumbe
alikuwa amechezewa maindi tu.
Mnanyaka masela unajua kwenye hili laifu siyo
ishu kuringia uzuri na kushindwa kujikontroo. Ni
beta mazee mtu ukaringia bahati na siyo kitu cha
sura na umbo bomba.
Ona sasa, pamoja na ukare wa shori bati kitu cha
uchumba mwisho wa reli na laifu limestaki.
Mmenisoma washkaji zangu? Sii yuu neksti wik

Sunday, December 13, 2015

Soma

Kijana mmoja alitokea kumpenda sana dada mmoja ijapokuwa dada huyo alikuwa akimtolea nje mara kwa mara lakini kijana hakukata tamaa, akiendelea kurusha ndoano huku akiamini siku moja atafanikiwa.Siku moja dada huyo akiwa yupo nyumbani aliamua kumpigia simu huyu kaka na kumtaka aje nyumbani kwake, yule kijana alifurahi na kuhisi sasa ombi lake limekubaliwa.
Akiwa nyumbani kwake dada huyo , alikuwa amevalia kanga moja laini, kutokana na hali ya hewa ya joto la Dar es salaam.Kwa upande wa yule kijana alikuwa amefurahi sana na haraka alijiandaa na kuanza safari kuelekea kwa huyu dada, njia ni kaka huyu alikuwa akijiuliza maswali mengi, huku akiwa haamini kama yule dada amemuita nyumbani kwake. Alipofika, alibisha hodi na yuel dad a akafungua mlango huku akionyesha tabasamu pana katika paji la uso wake.
Kaka huyu aliingia ndani huku kijasho kikimteremka mithili ya mtu aliyekuwa anakimbia. Dada huyu alimkaribisha vizuri, yule kaka aliomba maji ya kunywa huku muda wote akimtizama kwa umakini dada huyu mrembo, aliyeumbika kila idara na ile kanga nyepesi aliyovaa ilikuwa ikionyesha umbo zuri la dada huyu ambaye waswahili huwa wanasema, mtoto kajaaliwa (mashalaah) Kaka alikuwa akivuta pumzi kwa haraka haraka, na kusema "Nimefurahi sana, umenikaribisha nyumbani kwako ni pazuri sana." Yule dada alitabasamu na kusema "Asante sana, nimefurahi pia umeitikia wito wangu, samahani kwa usumbufu wangu".
Yule kaka alitabasamu huku akijisogeza sogeza "Hakuna tatizo, usijali kabisa, mimi nipo kwa ajili yako, naimani sasa nina...." Kabla hajamilizia kuongea yule dada alimshika mikono yake miwili huku akimtizama machoni, kwa macho yake malegevu, mithili ya mtu aliyekula kungu "Samahani kaka, mimi nimekuita hapa kuna jambo nataka unishauri, nataka kujua ni zawadi gani nzuri unaweza kumpatia mwanaume unayempenda" Kaka yule alikuwa akitetemeka na kusema "Chochote tu, zawadi ni zawadi, alimradi kuwe na mapenzi ya kweli" Dada yule alitabasamu na kusema "Ni kweli, mapenzi ya kweli ndiyo jambo la msingi, nitampenda maisha yangu yote" Kaka yule akauliza "Utampenda? Nani huyo"
.
Yule dada alitabasamu tena na kusema "Samahani, rafiki nilikuwa sijakuambia, wiki ijayo nafunga ndoa na mpenzi wangu wa muda mrefu ambaye nampenda sana, na pia nilikuita ili nikupe kadi ya harusi, nitafurahi kukuona, kwani wewe ni rafiki yangu pia" Yule kaka alibaki amepigwa na butwaa, "Ati, nini unaolewa, daaah, jamani, kwahiyo." Alinyanyuka na kuondoka bila ya kuaga huku akimuacha yule dada anamuita ili ampatie kadi bila ya mafanikio.
SIYO KILA UNACHOKIWAZA MOYONI MWAKO KITATOKEA KAMA UNAVYOTAKA. KWAHIYO NI VYEMA KUJIANDAA KUKUBALIWA AU KUKATALIWA
FACEBOOK
“"Reshmail Manyama want to be your friend.'confirm' 'ignore' ulikuwa ni ujumbe ambao macho yangu yalikutana nao nilipofungua mtandao wa kijamii wa ‘facebook’,sikumbuki kama nilijifikiria mara mbili kwani niliona ni jambo la kawaida sana kukutana na 'notifications’ kama hizo,na mara zote neno confirm(kubali) lilipata fursa ya kutumika.hivyohivyo hata kwa Reshmail nilifanya hivyo."You and reshmail are now friends" ndio ujumbe ulionisindikiza baada ya kukubali ombi lile kutoka kwa Reshmail.
* * * * *
Ni kijana mtanashati niliyebahatika kukutana nae pale chuo kikuu cha mtakatifu Augustine Mwanza,alijipenda kuanzia ndani ya chumba chake hadi mwili wake,ilikuwa ni nadra sana kumfumania akiwa amevaa nguo aliyoivaa jana,bila kumnyima haki yake nasema alikuwa anapendeza kila siku,macho yangu ya kipelelezi na kamera zangu za kipaparazi kamwe hazikufanikiwa kumjua aliyekuwa ubavu wa pili wa bwana huyu yaani 'MPENZI'. Ukipenda waweza kuniita kimbelembele lakini ukiniita hivyo basi majina hayo yatakuwa mengi pale chuoni kwani wengi walikuwa na shauku kubwa ya kujua siri hiyo na kamwe hawakufanikiwa.
Binadamu hatuna dogo watu washaanza kusema eti huenda jamaa ana matatizo makubwa tu mwilini mwake ndio maana yuko peke yake licha ya kushobokewa na wasichana warembo, mh! mimi sikuwa mmoja wao lakin nilijiuliza pia kulikoni??
Makala mbovu zilizokuwa zinaandikwa na gazeti la chuo lililojulikana kama ‘Saut voice’ ndo zilinizonivuta zaidi kutaka na mimi siku moja kuandika katika gazeti hilo lililokosa mvuto siku za hivi karibuni makala nzuri itakayorudisha heshima ya gazeti hilo.Taratibu nilijenga mazoea na hatimaye nikafanikiwa kumzoea "THE MOST WANTED" ucheshi wangu ndio uliomvutia zaidi kupenda kuwa karibu nami pamoja na mchezo wa mpira wa miguu kwani wote tulikuwa mashabiki wakubwa,haukupita mwezi mzima nikawa nina uwezo wa kuanza kazi yangu,ni mimi na Adam Michael kwenye meza moja chumban kwangu ananipa hadithi yake ya maisha yaliyomfanya awe kama alivyo.
"Aah!! jamani Reshmail..." alianza Adam,yangu masikio na macho nikaanza kusikiliza kwa makini.
** ** **
Hadithi ya Joka Jeupe
K atika enzi za kale, kwenye Mlima wa Emi kulikuwa na majoka mawili yenye umri wa miaka elfu moja, moja jeupe, moja jeusi. Majoka hayo mawili yalipenda sana mandhari ya watu wanapoishi, basi yalijibadilisha kuwa wasichana wawili warembo, moja lilijipa jina la Bai Suzhen
, jingine liliitwa Xiao Qing. Siku moja walifika kwenye sehemu maarufu yenye mandhari nzuri, ziwa la Xihu mjini Hangzhou.
Mandhari ya ziwa la Xihu kweli ilivutia sana, walipofika kwenye daraja moja la ziwa hilo ghafla mvua ilianza kunyesha, wakakimbia mvua na kujificha chini ya mti mmoja mkubwa. Wakati huo alikuja kijana mmoja mwenye mwamvuli aliyeitwa Xuxian, ambaye alikuwa akirudi nyumbani baada ya kusafisha makaburi. Alipoona wasichana chini ya mti aliwasaidia kwa mwamvuli wake na baadaye aliwasaidia kuwapeleka nyumbani kwa mashua. Bai Suzhen alianza kumpenda kijana huyo, alipoagana na kijana huyo alimwambia kesho aje kuchukua mwamvuli wake.
Siku ya pili kijana Xuxian alifika nyumbani kwa Bai Suzhen karibu na ziwa kuchukua mwamvuli wake. Bai Suzhen alimshukuru sana na kumwuliza habari za familia yake, akafahamu kuwa alifiwa na wazazi wake mapema tokea alipokuwa mtoto na sasa anaishi kwa dada yake na kufanya kazi katika duka moja la dawa. Msichana Bai Suzhen aliomwomba aolewe naye. Hakika Xu Xian alikuwa na furaha isiyo kifani. Kwa kuongozwa na Xiao Qing walifanya sherehe ya ndoa. Baada ya ndoa walianzisha duka la dawa. Bai Suzhen alifahamu matibabu, kila siku aliwatibu wagonjwa wengi.
  Kulikuwa na sufii mmoja wa dini ya Buddha aliyekuwa anaitwa Fa Hai. Fa Hai alikuwa anajua siri ya Bai Suzhen kuwa alikuwa joka mwenye miaka elfu moja, na hakika angewadhuru watu, hivyo alidhamiria kumwokoa kijana Xu Xian.
Siku moja Fa Hai alikuja nyumbani kwa Xu Xian, alimwambia, mkewe ni zimwi. Xu Xian hakuamini. Basi Fa Hai alimwambia, kama haamini, ajaribu kumshawishi anywe pombe tarehe 5 Mei, siku ya mashindano ya mbio za mashua, na kama akinywa atarudia asili yake.
Tarehe 5 Mei ilifika, kila familia hunywa pombe kusherehekea siku hiyo. Majoka yanaogopa pombe, Bai Suzhen alitaka kwenda mlimani kukwepa, lakini alikuwa na wasiwasi kuwa mumewe Xu Xian atamshuku, alikuwa hana budi ila kubaki nyumbani akijidai anaumwa.
Ingawa Xu Xian hakuamini aliyoambiwa na sufii Fa Hai, lakini kila mmoja katika siku hiyo hunywa pombe, hivyo alimshawishi mkewe anywe pia. Mkewe Bai Suzhen alishindwa kukataa, alikunywa glasi moja, mara akaanza kuona kizunguzungu. Xu Xian alimsaidia hadi kitandani, kisha akaenda jikoni kumtengenezea supu ya kuondoa ulevi. Akaja na bakuli moja la supu kitandani, alipofungua chandarua akaona joka kubwa jeupe limelala kitandani, Xu Xian alikufa kwa mshtuko.
Joka jeupe lilipozinduka likaona mumewe amekufa kwa mshtuko, alihuzunika sana, alimwomba Xiao Qing amtunze mumewe, na yeye akatoka haraka na kwenda kwenye mlima mmoja ulioitwa Xianshan ambako kulikuwa na aina moja ya jani la dawa ambalo lingeweza kumwokoa mumewe.
Wakati huo Bai Suzhen alikuwa amepata mimba ya miezi saba. Alipofika mlima Xianshan watoto waliokuwa wananlinda mlima walipojua kuwa anataka kuiba jani la ajabu walipambana naye. Mungu wa mlima huo alipoona jinsi Bai Suzhen alivyohangaika kumwokoa mumewe alimpa jani la ajabu.
Xu Xian alifufuka, lakini bado alikuwa ameshikwa na hofu. Bai Suzhen alipatia mzungu wa kumdanganya, alitumia kitambaa kirefu cheupe na kukigeuza kuwa joka kuzunguka kwenye boriti la dari na kumwita mumewe aone. Kwa kuona joka hilo, Xu Xian aliondoa mashaka yake juu ya mkewe, na waliendelea kuishi kwa mapenzi.
Sufii Fa Hai hakukufa moyo. Siku moja alimdanganya Xu Xian kwenda kwenye hekalu lake na kumzuia asirudi nyumbani. Baadaye mkewe na Xiao Qing walikuwa kwenye hekalu wakitaka kumrudisha nyumbani, wakagombana na sufii. Wakati walipopurukushana, Bai Suzhen alisikia maumivu ya uja uzito, kwa haraka alirudi nyumbani na Xiao Qing, alipofika kwenye daraja alikumbuka jinsi alipokutana na mumewe na kuanza na mapenzi, alihuzunika sana. Xiao Qing alimlaumu Xu Xian kwa kumsikiliza sufii, alimshawishi Bai Suzhen amwache mumewe.
Kwa kusaidiwa na sufii wengine, Xu Xian alitoroka kutoka hekalu na kwenye daraja alimpata mkewe. Mkewe alimwambia ukweli wa mambo, kwamba kweli alikuwa joka. Wakati huo Xu Xian alikuwa ameelewa kwamba mapenzi ya mkewe ni ya kweli na makubwa, akamwahidi kuwa hatajali akiwa ni kitu gani, lakini ataishi naye mpaka kufa.
Baada ya kurudi nyumbani, muda mchache baadaye Bai Suzhen alizaa mtoto. Katika siku ya kutimiza mwezi mzima kwa mtoto walifurahi sana, lakini wakati huo sufii Fa Hai alikuja tena nyumbani, alimkamata Bai Suzhen na kumtia chini ya mnara wa Leifong kando ya ziwa la Xihu.
Xiao Qing alitorokea mlimani Emei, alijitahidi kuinua uhodari wake wa mapambano, mwishowe alimshinda Fa Hai, na alimwokoa Bai Suzhen.
SIMULIZI YA KWELI YA KUSISIMUA NA KUSIKITISHA YA MTOTO JANETH :
Kengele ya kutoka darasani iligongwa, wanafunzi wa shule ya msingi wakaanza kutoka madarasani huku wakifukuzana wengine wakipiga kelele ilimradi shwangwe tu.
Ilikuwa mara yangu ya kwanza kufundisha shule za hatua hiyo.
Ilikuwa ni shule ya serikali.
Jicho langu liliangukia katika sura ya msichana mdogo, nguo zake chafu. Alikuwa analia.
Alikuwa peke yake na hakuwa na yeyote wa kumbembeleza.
Mimi kama mwalimu sikutaka kujisogeza karibu naye sana. Kwanza nilikuwa mgeni.
Nikaachana naye.
Siku iliyofuata tukio kama lile likajirudia. Msichana yuleyule wakati ule uleule wa kutawanyika, alikuwa analia sana. Mwishowe aliondoka huku akiwa analia.
“Mbona mwenzenu analia?” nilimuuliza mwanafunzi mmoja.
“Huyo ni mama kulialia..” alinijibu huku anacheka.
Haikuniingia akilini hata kidogo kuwa yule binti analia bila sababu.
Siku ya tatu nikaanza kujiweka karibu naye.
Muda wa mapumziko nilimwita nikamnunulia chai, alikuwa ananiogopa na hakutaka kuniangalia machoni.
Sikumuuliza lolote juu ya tabia yake ya kulia lia kila anaporuhusiwa kurejea nyumbani.
Hata siku hiyo pia alilia vilevile. Wenzake wakawa wanamzomea.
Akili yangu iligoma kuamini kuwa binti yule analia bila sababu.
Kwanini alie wakati wa kutawanyika tu?? Hapana si bure.
Nikaendelea kujiweka karibu naye. Mkuu wa shule akafikishiwa taarifa kuwa nina mahusiano ya kimapenzi na yule mtoto.
Moyo wangu na Mungu pekee ndio walikuwa mashahidi. Nilikosa cha kujibu.
Nilijaribu kujiweka mbali naye lakini moyo ulinambia kuwa kuna jambo natakiwa kulijua.
Nikaendelea kuwa karibu naye. Hatimaye mkuu wa shule akanisimamisha kufundisha pale kwa tabia yangu ya kufanya mapenzi na mwanafunzi.
Nilijitetea lakini sikueleweka. Nikamwachia Mungu……
Licha ya kusimamishwa kazi, niliendelea kufuatilia nyendo za yule binti aliyeitwa Janeth.
Kila alipotoka shule nilimvizia njiani na kumnunulia chakula, kisha tunazungumza kidogo.
Aliponiamini kama kaka yake ndipo nikajieleza dukuduku langu.
“Janeth…” nilimuita.
“Bee kaka ….” Aliitika huku akinitazama.
“Nyumbani unaishi na wazazi.”
“Ndio naishi na mama..baba huwa anasafiri safari.”
“Mama yako ana watoto wangapi?”
“Mama yangu alikufa….alikufa nikiwa mdogo hata simkumbuki” Alijibu kwa sauti ya chini.
“Kwa hiyo unaishi na mama mdogo.”
“Ndio.”
“Unampenda mama mdogo?”
Swali hili likaikatisha furaha ya Janeth. Akaanza kulia, alilia bila kukoma, Janeth alilia kwa uchungu hadi nikajisikia vibaya. Nilimbembeleza kisha sikumuuliza tena.
Siku zikaenda bila kumuuliza chochote..
Baada ya siku kumi, ilikuwa siku ya michezo pale shuleni, hivyo hapakuwa na masomo.
Janeth alichelewa kuja shule, nilimngoja uwanjani, hadi alipofika majira ya saa nne.
Nikamwambia twende kunywa chai.
Siku hiyo nilimpeleka mbali kidogo, tukanywa chai, kisha tukakaa mahali palipokuwa wazi.
Nikaleta tena mjadala mezani.
Ni kuhusu maisha ya Janeth.
Alikataa kabisa kusema lolote, nilimshawishi sana.
“Usiogope mimi ni kaka yako.” Nilimpooza.
Janeth badala ya kusimulia akaanza kulia tena.
“Ataniua mama nikisemaaaa” alilalamika.
Nikambembeleza hatimaye akanieleza jinsi anavyonyanyaswa na mama yake.
“Mama hanipendi hata kidogo, ananipiga na kuninyima chakula, hapendi nije shule, vyombo tunavyotumia usiku hataki nivioshe usiku na hataki niwahi kuamka asubuhi, nikiamka natakiwa kufanya kazi zote, kufagia uwanja, kudeki nyumba, kuosha vyombo kisha ndipo nije shule. Baba akiwepo anajidai kunijali sana…”
Alijieleza.
“Ni hayo tu Janeth….niambie kila kitu.”
“Akijua ananiua alisema….”
“Kwani amewahi kukutesa vipi..”
Ni hapa Janeth alivyozungumza huku analia kilio ambacho hakitatoka masikioni mwangu kamwe.
Siku moja, alichelewa kuamka, ilikuwa siku ya mapumziko.
Mama yake alipomwamsha, aliitika na kupitiwa usingizi tena.
Mama aliporejea mara ya pili, alikuwa na mti mkavu, alimpiga nao kichwani na popote pale katika mwili, alipoona hiyo haitoshi akamvua nguo, akausokomeza katika sehemu za siri, aliuigiza hovyohovyo, ukuni huo ulikuwa wa moto.
Yeyote mwenye moyo wa nyama ajifikirie ukuni wa moto ukazamishwa sehemu za siri za mtoto wa darasa la sita.
Nilitokwa machozi.
Nikawahi kujifuta hakuona.
“Baba yeye alisemaje….”
“Baba ni mkali na hapendi kunisikiliza na mama aliniambia nikiambia mtu ananiua mara moja.” Alijibu kwa huzuni.
“Nikija na dada yangu tunaweza kukuona ulivyounguzwa..”
“Ndio…” alinijibu.
Sikutaka kulaza damu nikampigia simu rafiki yangu wa kike.
Nikamuuliza kama yupo kwake, alikuwepo.
Nikaongozana na Janeth.
Tukafika, Janeth akatoa nguo zote.
Ilihitaji moyo wa kiuaji sana kutazama mwili wa Janeth mara mbilimbili.
Alitisha, hakika alikuwa ameunguzwa vibaya na vidonda vilikuwa havijapona vizuri.
Dada yule alishindwa kujizuia alimlazimisha Janeth twende kwa mama yake amkabiri na kumpa kipigo. Nikamzuia.
Hata mimi nilikuwa na hasira kali. Lakini sikutaka kuiruhusu ifanye kazi.
Nikachukua kamera, nikampiga picha Janeth katika yale makovu.
Mbio mbio nikaenda polisi, kituo cha haki za watoto nikaelezea mkasa ule huku nikishindwa kujizuia machozi.
Nikawaonyesha na picha.
Tukaongozana nao hadi nyumbani kwao Janeth.
Mama yule akakamatwa bila kutarajia.
Nilitamani kumrukia nimng’ate lakini haikuruhusiwa.
Sheria ikafuata mkondo. Janeth akaanza kupokea tiba.
Yule mama akahukumiwa kwenda jela miaka sita..hadi sasa yupo jela.
Mume wake alitozwa faini kubwa kwa kosa la kutofuatilia maendeleo ya mtoto wake kiafya……..
Mimi nilirudishwa kazini, kwa heshima kubwa. Heshima ya nkumkomboa mtoto.
***Akina JANETH wapo mtaani kwako…..usiwaangalie na kuwaacha tu…hebu jaribu KUWA SAUTI YAO….hawawezi kusema…hebu sema badala yao…….wanalia kisikie kilio

MakAburi ya nungwi

Mwangwi wa vilio na simanzi kutoka kwa watu waliopoteza maisha baada ya meli kuzama kwenye mkondo wa bahari wa Nungwi, Zanzibar uliambaa kwenye maji na kwenda kugota kwenye ukuta wa chini ya bahari, mahali palipokuwa na maelfu ya makaburi yalichongwa kwenye mwamba mgumu kuhitimisha safari ya wote waliopoteza maisha yao kwenye ajali hiyo ya kihistoria.
Kwa binadamu wa kawaida, wenye macho yanayoweza kutofautisha giza na mwanga pekee, hiyo ilikuwa ni ajali ya bahati mbaya kama zilivyo ajali nyingine lakini kwa wale wenye uwezo wa kuona zaidi ya upeo wa kawaida wa binadamu (beyond normal vision), haikuwa ajali ya bahati mbaya bali kitu kikubwa zaidi kilichopangwa na kuratibiwa kwa umakini wa hali ya juu.
“Babu! Mbona nasikia vilio vya watu wengi sana! Kwani kuna nini?” kijana mdogo anayefundishwa imani za kishirikina, Kahungo alikuwa akimuuliza babu yake.
“Hivyo ni vilio vya roho zilizopokonywa miili yao bila kujiaanda.“
“Unamaanisha nini babu?”
“Ili binadamu akamilike anapaswa kuwa na mwili na roho, vitu hivi vinapotengana, binadamu hufa. Sasa hawa wametenganishwa miili na roho ghafla kwenye ajali bila hata kujiandaa na ndiyo maana wanalia sana.”
“Sasa mbona wanazikwa wakiwa hai? Kwa nini wengine wanalia sana wakati wengine hawalii? Na hawa waliokuwa wanachimba makaburi huku chini ya bahari walikuwa wanatumia vifaa gani?”
Hawazikwi wakiwa hai. Zile unazoziona ndiyo roho, zinapambana kurudi kwenye miili yao inayoelea juu ya maji lakini zinashindwa. Wanaolia sana ni wale ambao kwenye maisha yao walimsahau Mungu na wakazama dhambini! Wale unaowaona hawalii ni wale ambao walikuwa wanafuata maagizo ya Mungu. Waliochimba makaburi haya ya Nungwi walitumia kitu chepesi sana, walitumia maarifa ya giza!”
“Maarifa ya giza? Lakini mbona hata misalaba inayowekwa kwenye makaburi haya siyo kama ile tuliyozoea kuiona kule duniani? Naona kama ni mifupa ya binadamu imefungwa na kutengenezwa misalaba,“ Kahungo alizidi kumhoji babu yake kwani kila alichokuwa anakiona kilikuwa kinamshangaza.
“Hizi ni kanuni za nguvu za giza! Mbona hushangai mimi na wewe kufika huku chini ya bahari bila ya kuwa mitungi ya gesi wala nini na bado tunapumua kama kawaida?”
“Mh! Kweli dunia ina mambo. Halafu nilisikia kuna wazamiaji kutoka kusini mwa Afrika walishindwa kufika huku, mbona sisi tumefika kirahisi na bado naona watu wengi tu wakiendelea na shughuli za mazishi?”
“Hii dunia mjukuu wangu tunafaidi sisi wenye nguvu za giza! Hakuna kinachotushinda na ndiyo maana nataka nikuandae na wewe ufuate nyayo zangu, si unaona mimi nimeshakuwa mzee! Kuna kazi sana mpaka kufikia huku tulipo, unabidi uvuke ngazi nyingi sana. Wengi hata ngazi ya kwanza hushindwa kuivuka.”
“Kwani hapa tulipo panaitwaje babu?”
“Nungwi! Kuna mkondo bahari wenye nguvu sana hapa na kuna wakati maji huwa yanachemka. Kutokana na maajabu ya hapa ndiyo maana wachawi waliamua kuweka kituo chao kikuu. Maji yanapishana kwa ngazi kuanzia juu hadi chini.
“Unataka kusema hiki ni kituo cha wachawi?”
“Eee! Wengi watashangaa kwa sababu ya ajali iliyotokea, lakini ukweli ni kwamba Nungwi ipo kwa miaka mingi iliyopita. Hii siyo ajali ya kwanza kutokea hapa. Mimi tangu nikiwa mdogo nilikuwa nakuja hapa kuongeza nguvu za kichawi na nilikuwa nikishuhudia ajali kubwa kuliko hata hii.”
Maelezo ya babu yake yalimshangaza mno Kuhungo. Alizoea kusikia au kusoma hadithi za kutisha kwenye vitabu lakini sasa alikuwa eneo la tukio akishuhudia mwenyewe kila kitu. Babu yake akazidi kumfafanulia mambo.
“Siyo binadamu wote unaowaona duniani wanaishi kihalali, wengi hawafuati maagizo na mafundisho ya Mungu! Wanavunja amri zake kwa makusudi. Wanaabudu sanamu na kutukuza dhambi! Hawaogopi kufa wala adhabu za kaburi! Watu kama hawa wakiingia kwenye mitego ya nguvu za giza hawaponi!
“Sisi (wachawi) huwa tunasaidia kuwafikisha kwa urahisi kuzimu kwa kuwapitisha kwanza kwenye malago ya wachawi ambapo hutumikishwa kwa kipindi fulani kisha kuachwa waendelee na safari zao. Miongoni mwa njia za kuwasaidia wafike upesi kwenye safari zao ni kuwazika chini ya bahari.
“Babu! Unataka kusema makaburi chini ya bahari hayapo hapa Nungwi pekee?”
“Yapo sehemu nyingine nyingi, lakini kwa miaka mingi hapa ndiyo kwenye makaburi maarufu na mengi zaidi, ndiyo maana hata mkondo bahari wa hapa una nguvu kubwa na husababisha ajali nyingi na kubwa kuliko sehemu nyingine.”
“Aaah! Mbona unanichanganya! Kwani kilichoanza kuwepo hapa Nungwi ni makaburi ya chini ya bahari au mkondo wenye nguvu unaosababisha ajali?”
Swali lile lilimfanya yule mzee amkazie macho mjukuu wake huku akiwa ni kama ambaye hakutegemea kulisikia kutoka kwake. Aliachia tabasamu hafifu kisha akasema:
“Naona umekua siku hizi mjukuu wangu kwani unauliza maswali ambayo hata mimi nilipokuwa na umri kama wako sikuweza kuyafikiria. Kwa kuwa una hamu ya maarifa juu ya ulimwengu usioonekana kwa macho ya kawaida, nitakufafanulia kila kitu.”
“Cha kwanza kuwepo ilikuwa ni kituo kikuu cha wachawi miaka mingi sana iliyopita. Kutokana na nguvu za giza zinazozalishwa chini ya bahari kila wachawi kutoka sehemu mbalimbali wanapokutana, maji yalikuwa yakivurugika sana na kuchemka, ndiyo mkondo wa bahari ukaanza kutokea taratibu kisha ukawa unazidi kuongezeka nguvu.
“Mkondo huo ulianza kusababisha ajali nyingi kwa wasafiri wa majini na kupoteza maelfu ya roho za watu, waliokuwa wanakufa wakawa wanaletwa kuzikwa huku chini, ndiyo yakatokea makaburi haya ambayo yalizidi kuongezeka wingi kwa kadiri ajali zilivyokuwa zinazidi kutokea.”
Baada ya kukaa kule chini ya bahari kwa saa nyingi. Kahungo akishuhudia mauzamauza mengi ya kichawi, alimuomba babu yake waondoke kwani moyo wake ulishindwa kuvumilia yale aliyokuwa anayaona na kuyasikia. Wakashikana mikono na babu yake kisha wakafanya ishara za kichawi, Kahungo akaambiwa afumbe macho kama alivyofanya awali wakati wa kuja. Kufumba na kufumbua wakajikuta wako mchangani, ufukweni mwa bahari.

Friday, December 11, 2015

Download latest song of diamond platnumz

Utanipenda just bofya hapa

Download justin beiber sorry

"Sorry"
You gotta go and get
Angry at all of my honesty
You know I try but I don't do too well with
apologies
I hope I don't run out of time, could someone call
a referee?
Cause I just need one more shot at forgiveness
I know you know that I
Made those mistakes maybe once or twice
And by once or twice I Mean
Maybe a couple a hundred times
So let me oh let me
Redeem oh redeem oh myself tonight
Cause I just need one more shot at second
chances
Yeah
Is it too late now to say sorry?
Cause I'm missing more than just your body, ohh
Is it too late now to say sorry?
Yeah I know that I let you down
Is it too late to say I'm sorry now?
I'm sorry yeah
Sorry yeah
Sorry
Yeah I know that I let you down
Is it too late to say I'm sorry now?
I'll take every single piece of the blame
If you want me too
But you know that there is no innocent one in this
game for two
I'll go I'll go and then
You go you go out and spill the truth
Can we both say the words, say forget this?
Yeah
Is it too late now to say sorry?
Cause I'm missing more than just your body, ohh
Is it too late now to say sorry?
Yeah I know that I let you down
Is it too late to say I'm sorry now?
I'm not just trying to get you back on me (oh, no,
no)
Cause I'm missing more than just your body (your
body), ohh
Is it too late now to say sorry?
Yeah I know that I let you down
Is it too late to say I'm sorry now?
I'm sorry (yeah)
Sorry (oh)
Sorry
Yeah I know that I let you down (let you down)
Is it too late to say I'm sorry now?
I'm sorry (yeah)
Sorry (oh)
Sorry
Yeah I know that I let you down (let you down)
Is it too late to say I'm sorry now?

Top 40


1
Hello
Adele





2
Sorry
Justin Bieber



3
Hotline Bling
Drake

Watch 


4
What Do You Mean?
Justin Bieber

Watch 


5
The Hills
The Weeknd

Watch 


6
Stitches
Shawn Mendes

Watch 


7
Love Yourself
Justin Bieber




8
Here
Alessia Cara

Watch 


9
Like I'm Gonna Lose You
Meghan Trainor Featuring John Legend

Watch 



10
Same Old Love
Selena Gomez

Watch 

THIS WEEK IN
1
Blank Space
Taylor Swift

11
679
Fetty Wap Featuring Remy Boyz



12
Ex's & Oh's
Elle King

Watch 



13
On My Mind
Ellie Goulding

Watch 


14
Wildest Dreams
Taylor Swift

Watch 



15
Jumpman
Drake & Future



16
Can't Feel My Face
The Weeknd

Watch 


17
Focus
Ariana Grande



18
Watch Me
Silento




19
Antidote
Travi$ Scott



20
Lean On
Major Lazer & DJ Snake Featuring M0




21
Confident
Demi Lovato




22
White Iverson
Post Malone




23
Die A Happy Man
Thomas Rhett




24
Don't
Bryson Tiller

Watch 


25
Locked Away
R. City Featuring Adam Levine

Watch 



26
All I Want For Christmas Is You
Mariah Carey

Watch 


27
Perfect
One Direction



28
Trap Queen
Fetty Wap




29
Where Ya At
Future Featuring Drake




30
Say It
Tory Lanez

Watch 


31
Where Are U Now
Skrillex & Diplo With Justin Bieber




32
Break Up In A Small Town
Sam Hunt



33
Drag Me Down
One Direction

Watch 


34
I'll Show You
Justin Bieber

Watch 


35
Hit The Quan
iLoveMemphis

Watch 



36
Roses
The Chainsmokers Featuring ROZES

Watch 



37
In The Night
The Weeknd



38
Good For You
Selena Gomez Featuring A$AP Rocky

Watch 


39
See You Again
Wiz Khalifa Featuring Charlie Puth



40
Renegades
X Ambassadors

Burundi

Heavily armed attackers have launched co-
ordinated assaults on several army barracks in
Burundi.
At least seven people, including some attackers,
have reportedly been killed in Bujumbura, the
capital.
Witnesses described hearing gunfire and
explosions for several hours, in Musaga in the
south and Ngagara in the north.
The incident is the worst violence since an
attempted coup in May, sparked by President
Pierre Nkurunziza's third-term bid.
Attacks: Latest updates
Is Burundi on verge of return to ethnic conflict?
Tit-for-tat killings spread fear
Bujumbura residents have taken cover at home and
are too frightened to go to work or send their
children to school, reports the BBC's Prime
Ndikumagenga from the city.
The attacks are the first on military targets since
the coup attempt, he says.
A presidential adviser said that government
opponents had been trying to create a diversion to
free prisoners with the attacks, but had failed.
Mr Nkurunziza won a disputed election in July.

Thursday, December 10, 2015

Roberto in dodoma

Mwanamuziki na mtangazaji wa redio, Roberto
Chindaba Banda ‘maarufu Roberto Amarula kutoka
nchini Zambia (katikati), akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
leo, kuhusu onyesho lake atakalolifanya leo katikka
fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar es
Salaam na kesho ukumbi wa Ngalawa Pub mkoani
Dodoma katika Tamasha la Instagram Party
Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Freconic Ideaz, Fred Ngimba ambao wamemleta
msanii huyo hapa nchini kwa kushirikiana na
Kampuni ya C&G Solutions na kulia ni Mwanamuzi
David Banda ‘General Ozzy kutoka Zambia.