Inakuwa nene masela wangu? Kipande hii ni mzuksi
kichizi arifu. Kama vipi welikamu kwa sana kwa fasi
ya hapa jamvini tukisanue mazee ama nini! Basi
sawa.
Wanangu kuna ishu zingine hazihitaji mtu kuwa
machi noo kozi kuna pipo ni mamasta maindi ileile
na ukileta za kujua sana dheni watu wanakupiga
chabo dheni wanakuchora tu si unajua zile? Kuna
wale makaksi wa ukwehe ambao mara nyingi siyo
wachangiaji wa mamada kiivo bati wana madini ile
mbaya kwa kichwani! Ebana kitu cha holidei ya
uhuu vepe? Mambo ya foto kanga na ekotite
yalikuwa mpango mzima? Barida!
Basi bana huku na huku selaa wangu akamingo na
chiki mmoko mkare aibu kiaje sasa mazee. Yaani
usipimie kabisa kwa jentromani wa ukwehe achana
na wale watoto mayai lazima uzime fegi kachala
wangu.
Siyo siri wanangu mtoto ni sumu ile mbaya sema
tu laifu lake huko nyuma lilikuwa la kukurukakara
za hapa na pale wanangu wenyewe kwenye
mambo yaleee ya kubadili mameni kama chizi
f’lani hivi freshi.
Laifu limemuvu fasta na huwezi kubilivu si ndo
msimu wa kitu cha holidei? Masela hii siyo taimu
ya kumbwela ni mwendo wa maandalizi ya kufa
mtu ili wanangu wasiaibike.
Unaambiwa jamaa yangu kazama ofisini kwa shori
hapo dauni tauni Bongo tambarare kupata sevisi
f’lani si ndo kachaa kadata na mtoto? Akaona
isiwe kitu, baada ya kitambo f’lani hivi mwana
akatangaza kuweka kitu na boksi ndani.
Sasa bana unajua ukitaka kugonga bata la holidei
usimchunguze sana kozi hutalila kwa raha au
hutalila kabisa. Basi bana, kabla ya kumweka kwa
skani akaona amwekee spai wa kumchunguza
kama ametulia au ndo kama hivo magumashi?
Yule msela aliyepandikizwa na mwana si ndo
akaanza mbishe za kumfukuzia shori? Kama
nilivyokuteli bifoo kwamba tabia ni kama rangi
kuifuta ina kosti zake. Jamaa kamuimbisha shori
hadi wakakubaliana wakafanye yao kwa hoteli!
Da! Noma sana wanangu! Shori amefika kwa
mapokezi kakaribishwa freshi na bashasha za
kumwaga kisha akapewa funguo za rumu.
Mazee wakati shori anamsikilizia jamaa akiwa
amejimwaga kwenye peji ndani ya suti ya kuzaliwa,
ghafla bin vuu mlango ukagongwa…kwenda
kufungua shori hakuamini macho yake kukutana
feisi kwa feisi na mchumba’ke orijino kumbe
alikuwa amechezewa maindi tu.
Mnanyaka masela unajua kwenye hili laifu siyo
ishu kuringia uzuri na kushindwa kujikontroo. Ni
beta mazee mtu ukaringia bahati na siyo kitu cha
sura na umbo bomba.
Ona sasa, pamoja na ukare wa shori bati kitu cha
uchumba mwisho wa reli na laifu limestaki.
Mmenisoma washkaji zangu? Sii yuu neksti wik